BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, August 12, 2010

MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA YATAKIWA KUWALIPA FIDIA WAKAZI WA NDUMI TANGA!

WAZIRI wa miundombinu Dkt Shukuru Kawamba ameitaka mamlaka ya Bandari kuharakisha malipo ya wananchi waliochukuliwa maeneo yao kwa ujenzi wa Bandari mpya wa eneo la Ndumi ambapo hekta 82 zinahitaji kufidiwa ili kuepusha migogoro.

Dkt Kawambwa alikuwa jijini Tanga kwa ajli ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya usalama barabarani na wiki ya nenda kwa usalama iliyofanyika kitaifa mkoani Tanga,alisema ili kuondoa dhana ya ujenzi bandari ya Tanga ni hadithi wananchi wanapaswa kufidiwa.

Pamoja na agizo hilo kwa mamlaka ya bandari,Waziri Kawambwa alisema yeye na wizara yake itahakikisha kwamba inalisimamia suala hilo ili kuweza kuharakisha ulipwaji wa wananchi sambamba na mchakato wa ujenzi wa bandari hiyo ya Ndumi.

"Mimi kama waziri mwenye dhamana nitahakikisha utekelezaji unakuwepo zoezi la ujenzi wa bandari hii mpya,pia nitahakikisha ujenzi wa miundombinu mingine kama ya reli ya Tanga Arusha na Arusha Musoma unatekelezwa"alisema Waziri Kawambwa.

Hata hivyo waziri Kawambwa alisema kwamba utekelezwaji wa miradi hiyo ni mpango wa serikali katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi CCM katika sehemu ya ahadi zake ilizowaahidi wananchi ambapo wamedhamiria kwa dhati kukamilisha suala hilo.

Pia aliwataka wananchi kuwa na subira kuhusiana na ujenzi wa bandari mpya kuhusiana na upitikanaji wa michakato mbalimbali ili kuweza kuwa na umakini wa suala zima la jenzi wa Bandari ya Ndumi sambamba na uimarishaji wa miundombinu ya reli nchini.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari nchini,Julius Mfuko alisema mchakato wa ulipaji umeshaandaliwa na miezi mitatu kuanzia sasa utaanza kulipwa na miezi mitatu kuanzia sasa wananchi wataanza kulipwa na Bil 1.7 zimetengwa kwa ajili ya malipo.

Alisisitiza kuwa mamlaka ya bandari tayari imeandaa upembuzi yakinifu ambapo dola mil 695.5 zimetengwa ili kufanikisha ujezi wa bandari mpya na mil 500 ndizo zilizofanya upembuzi yakinifu ambapo yanasubiriwa maelekezo ya wizara ya miundombinu.

Mfuko alibainisha kuwa kwa upande wa mamlaka ya bandari mchakato unaendelea vizuri ambapo wanasubiri serikali kupitia wizara yake ya miundombinu kuwapatia maelekezo ili ujenzi huo wa bandari uweze kufanyika haraka na kwa ufanisi na tija.

Na Sussan Uhinga,Tanga

No comments:

Post a Comment