BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, August 11, 2010

TDFA YAISHUKIA TFF!!!


Chama cha soka Wilaya ya Tanga TDFA (Tanga District Football Association) imeliomba shirikisho la soka hapa nchini TFF na chama cha soka mkoa TRFA kuangalia uwezekano wa kuzisaidia vyama vya soka wilaya ambazo zinakuwa na mzigo mkubwa wa kusimamia ligi bila ya kuwa na msaada.

Katibu Msaidizi wa chama hicho wilayani hapa, Salim Carlos aliiambia blog hii kuwa wilaya zimekuwa na mzigo mzito sana katika usimamiaji wa ligi ambazo zimekuwa na timu nyingi bila kupata msaada wowote.

Carlos alisema kuwa licha ya shirikisho hilo pia aliwataka wadau mbalimbali wa soka pamoja na wafanya biashara,wabunge na wakuu wa wilaya kusaidia vilabu mbalimbali vya soka katika wilaya zao na sio kukaa tu na kusema kuwa Tanga mpira umekufa hivyo wavisaidie vyama vya soka vya wilaya ili vionekane kama vilivyo vya wilaya nyengine.

Aidha alisema kuwa ili tatizo hili liweze kumalika katika wilaya na mikoa ni lazima shirikisho la soka hapa nchini liezekeze nguvu zake katika ligi za wilaya na sio kuangalia timu ambazo zinacheza ligi kuu kwa sababu mpira unaanzia chini.

No comments:

Post a Comment