BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, August 3, 2010

ROMA AWAKIMBIZA TENA FIESTA YA MWANZA!!

Kwa mara nyengine mkoa wa Tanga umezidi kung'aa kupitia mkali wa Hip Hop kutokea pande hizi ROMA kuzidi kuwakimbiza vilivyo wakazi wa Mwanza kunako Fiesta Jipanguse Rrrrrrrrrrrrrrrrrrr ya Clouds Fm ambayo kilele chake ni jumamosi hii ya tarehe 7 pale jijini Dar Es Salaam Leaders Club.

Roma ambaye safari hii alitoa fora pale alipowarushia mashabiki wake koti alilokuwa amevaa na kufanya umati mzima kulikimbilia kila mmoja akitaka liwe la kwake. Akizungumza na blog hii kwa njia ya simu R.O.M.A kwa maana ya Rymes Of Magic Attraction alisema kuwa, alifanya hivyo kutokana na shangwe za ukweli alizozipata punde tu alipokanyaga jukwaa. Na hiyo pia itakuwa kumbukumbu nzuri kwa shabiki wake atakayelichukua koti hilo. Pichani mashabiki wakigombea koti la msanii Roma

Roma akiwa kwenye picha ya pamoja na mashabiki wake mara baada ya kufanya makamuzi!

No comments:

Post a Comment