BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, August 31, 2010

NASSIR A.K.A 'OBAMA' KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM KOROGWE!

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, kushoto akiwa na mwenyekiti wa CCM Mkowa wa Tanga Mussa Shekimweli kulia wakati wakiwapungia wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo la Korogwe mji iliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mazoezi.

MWANAFUNZI wa Naibu waziri wa wizara ya habari na utamaduni Joel Bendera amepata ridhaa ya kupambana katika kinyang'anyiro cha ubunge kupitia CCM wilayani Korogwe. Nassir almaarufu "Obama" ndiye aliyependekezwa na CCM kuwania Ubunge Jimbo la Korogwe mji ambapo sasa atapambana na wapinzania ambapo hata hivyo ameeleza yafuatayo:-.

Katika sekta ya afya 'Obama" anasema amekusudia kutumia mpango wa ushirikishwaji jamii ili kupanga mbinu shirikishi katika kupambana na adui maradhi wilayani humo. Amekusudia kupambana kwa hali na mali kuhakikisha kwamba hospitali ya wilaya ya Korogwe "Magunga" inapandishwa hadhi na kuwa kama ile ya Tumbi wilayani Kibaha Pwani.

Obama "Yassin" ni mtaalamu wa manunuzi ya kimataifa na masoko ambaye alishawahi kufanya kazi shirika la maendeleo ya petroli TPDC kama mshauri mshawishi wawekezaji. Licha ya hilo "Obama"ni mjasiriamali aliye wekeza katika sekta ya kilimo na ameahidi kushirikiana na Mwalimu wake katika kuwapatia maendeleo wananchi wa wilaya ya Korogwe.

Katika mahojiano na mwandishi wa Makala haya,Obama "Nassir" anasema yeye ni mtoto tu ila ana mbinu na uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya ya Korogwe. "Nashukuru wanaCCM kunipendekeza kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM,la msingi ni mshikamano na ushirikiano...hii ndio mbinu sahihi ya kuwaletea maendeleo"alisema Nassir.

Nassiri ambaye amembwaga kwa mbali Mwalimu wake Joel Bendera anasema anamheshimu baba yake huyo aliyekuwa mwalimu wake kwani anafahamu jiografia ya wilaya hiyo. Kwa upande wa sekta ya afya Nassir anasema anakubali mchango mkubwa wa Naibu Waziri Joel Bendera ambapo akiingia madarakani atahakikisha anayaendeleza mazuri.

"Hebu angalia...'hospitali yetu ya Magunga,inapokea wagonjwa wengi lakini bado haiangaliwi kwa kina,suala la kupandishwa hadhi sio mjadala tena,inabidi tusaidiwe". "Kuna masuala muhimu hapa mfano miundombinu,kuongezewa wataalam wa sekta ya afya kama madaktari bingwa wa mifupa kwani ajali nyingi zinatokea na wanaletwa hapa"alisema.

Nassir anabainisha kuwa la msingi ni suala la utumiaji wa nguvu shirikishi kuiomba wizara ya afya kuboresha miundombinu ya hospitali ya wilaya ya Korogwe 'Magunga'. Akitanabaisha mazingira ya wilaya ya Korogwe Nassir anasema,mji huo una rasilimali nyingi ambapo kama dhana shirikishi itatumika ipasavyo basi maendeleo yatapatikana.

"Nguvu shirikishi ni tija,nakusudia kuwaletea wanachi fikra,matumaini,na maendeleo zaidi uheshimiwa uweze kukaa sawa katika kuwakomboa wananchi kwenye hali ya unyonge. Anafafanua usemi wake huo kwa kusema heshima ya CCM,wananchi na viongozi wake waliopo madarakani itapatikana iwapo maendeleo yatapatikana Korogwe.

Nassir anasema kwamba siasa ya sasa ni uchumi hivyo kuna kila haja kwa wale wanaopata nafasi kuwashirikisha wananchi katika kujikomboa na hali ya umasikini wa kipato. Hata hivyo Nassir anasema anakusudia kushirikiana na wananchi kuufanya mji wa Korogwe ulioko barabara kuu unaboreka kwa kutafuta wawekezaji watakauwezesha.

"Rasilimali watu na nyingine zilizopo zikitumika ipasavyo uchumi wa wilaya ya Korogwe na watu wake utaimarika, hivyo nasisitiza kwamba nitashirikiana na wananchi wangu".Nassir anaongeza kwamba haoni sababu ya kupanda gari lenye 'tinted' kujificha kwa wananchi ambapo kama mikakati kadhaa haijatekelezeka anakusudia kuwa muwazi kwa yote.

"Kwa nini nipande gari la 'tinted'yote tutakuwa tumepanga pamoja,kama tumefeli tunapeana mrejesho kila siku hivyo dhana hii shirikishi ndio nitakayoitumia"anamaliza. Pamoja na hayo hakusita kuizungumzia sekta ya michezo ambapo alisema atatumia uwezo na uzoefu wa Mwalimu wake Joel Bendera ili wilaya ya Korogwe irudishe hadhi yake.

"Mimi nitashirikiana na Mh.Bendera, anajua kila kitu hapa,ila lazima ieleweke kwamba burudani ni uchumi na ajira hivyo lazima iwepo tija"anabainisha Nassir. Akizungumzia mchakato wa ndani wa chama cha mapinduzi,CCM Nassir anasema umeboreka zaidi na tangu ameingia hajawahi kuona makundi wilayani Korogwe yanayoashiria chuki.

Aidha Nassir anakerekwa na suala la mimba za utotoni kwa wanafunzi suala ambalo kama ataingia kwenye ubunge ameahidi kulifanyia kazi ili liweze kukoma kabisa. Obama (Nassir) anashukuru wale aliyokuwa akipamba nao katika kuwania nafasi ya Ubunge kwa kumpongeza na kumpigia simu ila anasema amekosa mawasiliano na Mwalimu wake.

"Mh.Bendera sina simu yake na nadhani pia yeye hana yangu huyu ndiye hatuwasiliani ila wengine wamekuwa wakinipongeza na tutawasiliana na nakubali ushauri wao". Katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa Korogwe mji Nassir almaarufu 'Obama' alimgaragaza vibaya mwalimu wake Joel Bendera aliyemfundisha shule ya msingi ya Mazoezi Korogwe.

Nassir amezaliwa wilani Korogwe mwaka 1965 ambaye sasa ameingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kupambana na wapinzania kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.


Na Sussan Uhinga, Korogwe.

No comments:

Post a Comment