BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, August 3, 2010

JOH MAKINI NDIO MKALI WA HIP HOP TANZANIA KUPITIA ANKO MO BLOGSPOT!Msanii Joh Makini ndio ameibuka mshindi wa MKALI WA HIP HOP kupitia blog hii baada ya ushindani uliodumu kwa takribani miezi miwili. Makini ambaye alikuwa akichuana vikali na wasanii wengine wa hip hop nchini kama vile Chid Benz, Mwana FA, Ngwair, Fid Q na Prof Jay ameibuka na ushindi kwa jumla ya points 26 huku akifuatiwa na Chid Benz ambaye alipata points 19.

Fid Q kutokea Mwanza alipata nafasi ya tatu baada ya kupata points 18 huku Mwana FA akinyakua nafasi ya nne kwa kupata points 15, Prof Jay points 13 na Ngwair akipata points 9- hivyo kufanya jumla ya points zote kuwa 100.


Mpambano huu haukuwa rasmi...ilikuwa ni kutoa changamoto kwa wadau wa blog hii. Hapo awali ilishawahi kuwashindisha akinadada wanaofanya bongo flava nchini na hatimae Lady Jay Dee aliibuka mnyange. Shukrani wote ambao mlishiriki katika kupiga kura. Nawasihi endeleeni kutembelea blog yenu ya VIJIMAMBO VYA TANGA.

Kutokana na vuguvugu la uchaguzi mkuu nchini kote, nimeona niwaletee changamoto nyengine ya kutabiri ni nani ataibuka kidedea kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2010. Kuna vyama vinne..CCM, CHADEMA, CUF NA NCCR MAGEUZI- pigia kura chama unachopenda ili kiweze kuibuka mshindi kupitia blog hii.

Tazama poll hapo kulia pembeni palipoandikwa CHAMA GANI KUSHINDA UCHAGUZI MKUU 2010..? Asanteni sana.

No comments:

Post a Comment