BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, August 10, 2010

MFAHAMU MR EBBO KWA UNDANI ZAIDI!!!

ANKO MO: Tupe Historia ya Maisha Yako Kimuziki toka Ulikotoka mpaka hapa Ulipofikia

Mr Ebbo : Jina langu ni Abel Loshilaa Motika a.k.a Mr Ebbo, Nimezaliwa tarehe 26 may 1974 jijini Arusha. Elimu ya msingi nimeanza mwaka 1982 katika shule ya msingi kijenge baadae mwaka 1984 nikaamia tanga na kuendelea na masomo katika shule ya msingi nguvumali. Nakumaliza elimu ya msingi mwaka 1988.

Nikajiunga na elimu ya sekondari katika shule iitwayo jumuiya sec school. iliyopo jijini Tanga. Nilimaliza elimu ya sekondari mwaka 1992. Na kwa kipindi hicho chote wakati niko shuleni nilikuwa naimba kwaya kanisani. Kwenye kanisa la kisosora (lutheran church) ambapo ilinisaidia sana kujifunza muziki.

Nilirudi Arusha mwaka 1993 nikabahatika kupata kazi kwenye night club ambapo nilitumia mishahara yangu kurekodi nyimbo ambazo hazikunipa mafanikio yeyote isipokuwa ziliniweka katika ramani ya muziki mkoani kwangu. Baada ya hapo nilifanya kazi ya kuandaa matangazo ya biashara na vipindi vya redio kwenye studio iliyojulikana kama Supreme recording studios iliyopo mjini Arusha. kipindi hicho kilijulikana kama “Mambo gani haya” Nilirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikunipa mafanikio yoyote na hali hiyo ikanikatisha tamaa.

Baadaye mwaka 1995 nilipata kazi ya kuuza nguo kwenye duka la JJ BLACK lililoko jijini Arusha. Mwaka 1999 niliamua kurudi jijini Tanga nikafunga ndoa na kubahatika kupata watoto wawili Ashley na baadaye Alicia. Nilianza kazi ya uwakala wa kuuza magazeti mwaka 2000.Kazi ambayo pia haikuniletea mafanikio yeyote, baadaye mwaka 2001 nikaanzisha biashara ya kuuza mchele kwa jumla ambayo pia haikuwa na mafanikio yeyote. kipindi hicho chote nilipokuwa Tanga nilifahamiana na professor J. na Wagosi wa kaya, na wao pia walijua kuwa mimi ni msanii. Baaye nilijiunga na chuo cha kozi za computer jijini tanga.

Wagosi waliporekodi wimbo wao wa Tanga kunani , iliniamasisha ndipo nikaandika wimbo wangu wa Mimi mmasai mwaka 2002. Wimbo huo ukatambulisha Album yangu ya kwanza “ Fahari yako “ Baadaye mwaka 2003 nikafungua studio ( MOTIKA RECORDS) Ambayo imefanikiwa kuwatambulisha wasanii kama, Danny msimamo, Dr leader, Mo-kweli, na wengineo wengi , wote hawa niliwa produce mwenyewe. kama producer wa MOTIKA RECORDS.

Mwaka 2003 nikarekodi Album yangu ya pili iliyojulikana kwa jina la Bado ijasungumiswa. Mwaka 2004 nikarekodi Album yangu tatu iliyoitwa Kazi gani. Mwaka 2005 nikarekodi Album yangu ya nne iliyoitwa Alibamu. Mwaka 2006 nimerekodi Album yangu ya tano inayoitwa Kamongo.

No comments:

Post a Comment