BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, August 23, 2010

COASTAL UNION YALETA KOCHA MPYA KUTOKA MOMBASA


KLABU ya Coastal Union yenye maskani yake barabara ya 11 jijini Tanga imesajili kocha mpya kutoka Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu hiyo, Ahmed Aurora ameiambia blog hii kuwa tayari kocha huyo ameshawasili jijini hapa tayari kwa ajili ya kuanza kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na ligi daraja la kwanza.

Aurora alimtaja kocha huyo kuwa ni Saidi Ally kutoka Mombasa Kenya na kwamba ataanza rasmi kukinoa kikosi hicho kama kocha mkuu. Alisema kocha huyo awali kabla ya kwenda nchini Kenya alikuwa akiifundisha Klabu ya villa squad ambayo iliweza kupanda daraja kutokana na umahiri wa kocha huyo.

Aliongeza kuwa Kocha huyo na wachezaji 23 wapya waliosajiliwa na klabu hiyo watatambulishwa rasmi kesho( leo jumapili) kwa wanachama wa klabu hiyo katika mkutano wa pamoja utakaofanyika makao makuu ya klabu hiyo barabara ya 11.

Hata hivyo majaliwa ya kocha wa sasa wa klabu hiyo Mussa Ricco kuendelea kukinoa kikosi hicho bado hayajajulikana


No comments:

Post a Comment