BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, October 7, 2010

MWANAFUNZI WA ECKERNFORDE SEC SCHOOL ATOLEWA KWENYE CHUMBA CHA MTIHANI!

Mtahiniwa wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Eckernforde mkoani Tanga Zebida Mafuru ameondolewa ndani ya chumba cha mtihani ili asiendelee kufanya mitihani ya kidato cha nne inayoendelea Tanzania nzima kwa kuwa hana sifa ya kufanya mitihani hiyo.

Akiongea na Blog hii mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Eckernforde Salum Heri alisema kuwa mwanafunzi huyo aliondolewa chumba cha mtihani kwa kukosa sifa zinazositahili kufanya mitihani hiyo akiwa mtahiniwa wa shule kwani alifanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2006 jambo amabalo ni kosa kwa vigezo vya barazala mtihani.

Aliongeza kuwa kutokana na taarifa walizopata toka baraza la mtihani kuwa wanafunzi wote waliofanya mitihani ya kidato cha pili kabla ya mwaka 2007 hawatakuwa na sifa ya kufanya mtihani wa kidato cha nne wakiwa watahiniwa wa shule bali watafanya wakiwa watahiniwa wa kujitegemea.

Mwalimu mkuu aliendelea kusema kuwa alitoa taarifa hiyo kwa wanafunzi wote na kuwataka wale wote wasio na sifa wajitokeze ili tupeleke taarifa zao baraza na washughulikiwe ,walijitokeza wanafunzi kumi ambao hadi sasa wanaendelea kufanya mitihani yao wakiwa wanafunzi wa kujitegemea lakini mwanafunzi huyo hakuweza fanya hivyo hatukuwa na taarifa za yeye kufanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2006 na yeye mwenyewe alipinga hilo.

Mitihani ya kidato cha nne ilianza nchini kote oktoba 4 na jina la mwanafunzi huyo lilikuja pamoja na namba yake ya mtihani ambayo ni S698\113 pia kwa taarifa za mwalimu wake mkuu mwanafunzi huyo alifanya mitihani yote iliyoanza oktoba nne siku ya jumatatu yaani somo la Uraia na Hesabu.

Taarifa zaidi kutoka kwa mwalimu mkuu zinazidi kusema kuwa watahiniwa walianza na somo la jiografia na kuongeza kuwa cha kushangaza jina la Zebida halikuwemo kwenye orodha ya watahiniwa wa siku hiyo.

Juhudi za kumpata mwanafunzi huyo ili aongelee swala hili hazikuweza kuzaa matunda kwani alikuja kuchukuliwa mzazi wake mara baada ya kutokea kwa tatizo hilo .

No comments:

Post a Comment