BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, October 1, 2010

MASHIRIKA YA KIMATAIFA YASAIDIA KUENDELEZA UTALII PANGANI!

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) na mashirika mengine ya kuendeleza utalii duniani yamejitokeza kuisaidia sekta ya Utalii wilayani Pangani Mkoani Tanga ili iweze kutoa mchango mkubwa kwa mandeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Wadau wengine wa maendeleo Iikiwemo Shirika la utalii la Umoja wa mataifa (UNWTO),Kitengo umoja wa mataifa cha kuondoa umasikini kupitia utalii(STEP),Bodi ya Utalii nchini TTB,na Shirika la maendeleo la uholanzi (SNV),Umoja wa kuhifadhi mazingira duniani (IUCN) yamejitolea kukisadia kituo cha kuendeleza Utalii cha Pangani Coast Cultural Tourism Programme ili kuundeleza utalii uliopo wilayani humo

Mashirika hayo yamewezesha kupatikana kwa mafunzo mbalimbali kwa wananchi waishio Pwani ya bahari ya hindi,kutoa mikopo kwa vikundi vya kuendeleza utalii na kufanikisha kuanzisha huduma ya Mtandao wa Internet katika wilaya ya Pangani Mkoani Tanga sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya Kituo cha Kuendeleza Utalii cha Pangani Coast Cultural Tourism Programme kuanzisha huduma hiyo.

Kuanzishwa kwa huduma hiyo ya Mtandao imekuja siku chache baada ya Blog hii kuandika habari kuwa watalii wanaotembelea vivutio vya utalii wilayani humo wanalazimika kukatisha ratiba ya kukaa muda mrefu wilayani humo na kuishi kwa siku tatu kutokana na kutokuwepo huduma hiyo muhimu ya Mtandao wa Internet hali inayofanya Serikali kupoteza fedha nyingi zitokanazo na watalii hao.

Tatizo hilo lilikuwa linachangia kuididimiza sekta ya Utalii wilayani Pangani ambayo kwa kiasi kikubwa ina mchango mkubwa wa kuwaondoa wananchi katika lindi la umasikini unaowakabili kwa sasa


Mratibu wa Kituo cha Kuendeleza Utalii wa Utamaduni Wilayani humo cha Pangani Coast Cultural Tourism Programme,Bw Leonard Sekibaha alisema baada ya kuwepo tatizo hilo wahisani mbalimbali wamejitokeza kusaidia kituo hicho ili kiweze kutoa huduma hiyo.

Alisema kabla ya kuanzisha huduma hiyo juzi ya mtandao watalii walikuwa wakilazimika kutumia huduma hiyo ya Internet kwenye Hoteli za kitalii zilizopo wilayani humo mbapo gharama zake ni Dola 5 za kimarekani kwa saa hali inayowafanya watalii wengi kushindwa kumudu gharama hiyo.

Kwa sasa baada ya kuanzisha huduma hiyo,imerahishia watalii kupata huduma hiyo ambapo kwa sasa watalazimika kulipa sh.1,000 kwa saa tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wanalazimika kulipa dola 5 za Marekani

Alisema katika takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa watalii waliotembelea wilaya ya Pangani mwaka 2008 walikuwa ni 12,000 ambapo waliweza kuishi wilayani humo kwa muda wa siku tatu kutokana na kutokuwepo kwa huduma hiyo.

Aliwashukuru wahisani hao ambao wamejitokeza kusaidia kuendeleza sekta ya Utalii wilayani humo ambayo kwa sasa inazidi kutoa fursa nyingi hasa ajira kwa vijana.


No comments:

Post a Comment