MITIHANI ya Taifa ya Kidato cha Nne imeanza jana huku watahiniwa wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mitihani hiyo. Wakizungumza na Blog hii watahiniwa hao waliopo wamesema wamefanya mtihani wa Hisabati na Uraia na kwamba wanamatumaini makubwa ya kufanya vizuri.
Hata hivyo duru za elimu Mkoani Tanga hadi jioni ya jana zimearifu kutokuwepo kwa aina yoyote ya udanganyifu katika mitihani hiyo ya Taifa ya kidato cha nne. Afisa Elimu Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga Bwana Julius Mhanusi amesema hadi jioni mitihani hiyo imefanyika vizuri na kwamba hakuna dosari yoyote iliyoripotiwa.
Bwana Mhanusi amesema Serikali imejizatiti kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika vizuri bila ya kuwepo udanganyifu wa aina yoyote. Jumla ya watahiniwa 22,686 Mkoani Tanga wamefanya mitihani ya Taifa ya Kidato cha nne iliyoanza jana ambapo kati ya watahiniwa hao 19,552 wapo shuleni na 3,134 ni watahiniwa wa kujitegemea.
No comments:
Post a Comment