BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, October 5, 2010

MIGAHAWA, HOTELI ZAPEWA ONYO KALI NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA!


HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imewaonya wamiliki wa nyumba za kulala wageni,hoteli na migahawa kuhakikisha wanafuata kanuni za afya vinginevyo hatua za kuzifungia biashara hizo itachukuliwa.

Hatua hiyo ya Halmashauri ya Jiji imekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wananchi juu ya kutorodhishwa na huduma zinazotolewa na baadhi ya migawaha kukithiri kwa uchafu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bwana John Gikene amesema tayari ofisi yake imeshapokea malalamiko kutoka maeneo mbalimbali ya jiji juu ya kukithiri kwa uchafu huo.

Amesema kwa sasa Maofisa Afya wa Halmashauri ya Jiji wanaendesha msako ili kubaini hoteli,gesti na migahawa inayotiririsha maji machafu na kutozingatia kanuni za usafi.

Katika malalamiko hayo baadhi ya wananchi ni walelalamikia baadhi ya migahawa kutoa huduma kwenye mazingira ya uchafu hivyo kuleta hofu kwa watumiaji wa bidhaa za vyakula.


No comments:

Post a Comment