WAGONJWA wanaohudumiwa na Kituo cha Afya cha Ngamiani jijini Tanga wamelalakia upungufu mkubwa wa dawa unaokikabili kituo hicho hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa.
Wakizungumza na Blog hii baadhi ya wagonjwa wanaohudumia na kituo hicho wamesema inawalazimu kununua dawa madukani kutokana na baadhi ya dawa kukosekana kituoni hapo.
Wameiomba Serikali kukiwezesha kituo hicho kupata dawa wakati wote ili kupunguza adha hiyo. Akizungumzia malalamiko hayo Mkurunngenzi wa jiji la Tanga Bwana John Gikene amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kueleza kuwa inatokana na upungufu dawa kutoka bohari Kuu ya madawa MSD.
Aidha bwana Johna Dikene amesema kuwa halmashauri ya jiji la Tanga inachangia shilingi milioni 200 kwa ajili mfuko wa madawa hiyo serikali pekee haitoshelezi kutoa madawa katika jiji la Tanga.
Bwana Johna ameongeza kuwa njia rahisi ya kuondoa matatizo hayo katika zahanati hiyo ni tele kwa tele yaani kila kaya kuchangia shilingi elfu kumi.
Na Benedict Kaguo, Tanga
No comments:
Post a Comment