BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, October 1, 2010

WATOTO WA VIGOGO WATASOMA SHULE ZA KATA- MBARUKU

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Tanga mjini kwa tiketi ya CUF Bw.Mussa Mbaruku amesema atakapoingia madarakani atahakikisha watoto wa vigogo serikalini wote wanasoma shule za sekondari za Kata ili kuwezesha kupatikana msukomo wa kuziboresha shule hizo.

Akihutubia maelfu ya wananchi wa Jiji la Tanga katika uwanja wa Tangamano mbele ya mgombea Urais wa Chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba,mgombea ubunge huyo alisema kwa sasa Shule za sekondari za kata ziko kwenye hali mbaya kutokana na viongozi wa juu Serikalini hawasomeshi watoto wao katika shule hizo hivyo hawaoni uchungu wa kuziboresha.

Alisema atakapoingia bungeni atafuta matabaka na ubaguzi katika utoaji huduma za jamii kama vile elimu na Afya ili kuwawezesha wananchi wote kupata huduma sawa bila ubaguzi.

“Kwenye shule za serikali mazingira ya kujifunzia sio mazuri kabisa kutokana na kwamba serikali haiumii kwa kuwa watoto wao hawasomi shule hizo ,wote wanasoma shule binafsi sasa lini serikali itakumbuka kuboresha mazingira ya shule hizo”alisema Bw.Mbaruku

Alisema katika upande wa Afya atahakisha viongozi wote wa juu serikalini wanatibiwa katika hospitali za serikali ili kuwawezesha kuona umuhimu wa kuziboresha ili zitoe huduma sawa kwa wananchi wote.

Mgombea huyo wa Ubunge pia alisisitiza nia yake ya kuwasaidia wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mkoa wa Tanga kuweza kupata mafao yao ambayo alidai kuwa wamedhulumiwa.

Kuhusu fedha za wananchi zilizopotea kwenye upatu wa DECI ,Mgombea huyo aliahidi kufuatilia na kuihoji serikali iweje iseme mchezo wa DECI ulikuwa ni utapeli na batili ili hali ofisi zake zilifunguliwa na viongozi wa juu Serikalini.

“Kwa nini ofisi za DECI Tanga zilifunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mohamed Abdulaziz na kule Morogoro ilifunguliwa na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo nikifika bungeni nitahoji uhalali wa viongozi wa serikali kufungua ofisi hizo na kueleza kuwa ni za kitapeli”alihoji Mgombea huyo wa Ubunge.


1 comment:

  1. hongera sana Mh.MUSSA BAKARI MBAROUK. INSHALLA utashinda kwa kishindo

    ReplyDelete