BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, October 1, 2010

ZANTEL YASAIDIA VYAKULA WATOTO YATIMA MUHEZA!

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zantel imekabidhi msaada wa vyakula kwa kituo cha kulelea yatima cha Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu cha Kharia kilichopo wilayani Muheza Mkoani Tanga.

Akikabidhi msaada huo wa ngano,mafuta,unga Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo,Bi Sharon Costa alisema msaada huo wameutoa kama mchango wa kampuni hiyo kusaidia makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo Yatima.

Alisema jukumu la kuwasaidia yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo kampuni hiyo inaunga mkono juhudi hizo kwa kusaidia makundi hayo.

Alisema msaada huo unathamani ya Shilingi Milioni 1.1 na kuahidi kuwa kampuni hiyo itaendelea kusaidia makundi mbalimbali kwenye jamii kwani wateja wa kampuni hiyo ni jamii yenyewe.

Awali Msimamizi wa Masoko wa Zantel Mkoani Tanga Bw.Hamfrey Lyimo alisema baada ya kutembelea kituo hicho walibaini kuwepo changamoto zinazowakabili watoto hao ndio sababu waliamua kwenda kuwasaidia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo hicho Bi.Rehema Omari aliishukuru Kampuni hiyo na kutoa wito kwa jamii kuunga mkono juhudi za kuwasaidia yatima kwani watoto hao ni wa Taifa.

Na Benedict Kaguo, Muheza

No comments:

Post a Comment