BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, October 8, 2010

KAMATI YA MPIRA WA MIGUU WILIYA YA TANGA KUKUTANA!


KAMATI ya mashindano ya ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Tanga inategemea kukutana na kujadili mwenendo mzima wa ligi hiyo na hatua inayofuata.

Akiongea na Blog hii, katibu msaidizi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Tanga, Salim Kalosi amesema mkutano huo unategemewa kufanyika siku ya Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa soka mkwakwani saa nane mchana.

Kalosi ameongeza kuwa mkutano huo utakuwa wa awamu mbili ambao utashirikisha walimu na manahodha wa vilabu vinavyoshiriki ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Tanga

Katibu huyo msaidizi amesisitiza kwa washiriki hao kuzingatia maelekezo ya mwaliko ili waweze kuhudhuria kwa kufuata taratibu zilizowekwa na chama hicho na kuondoa mgongano na mkutano mwingine.


Na Sophia Wakati, Tanga

No comments:

Post a Comment