BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, October 11, 2010

HOSPITALI YA MAGUNGA WILAYANI KOROGWE YAKABILIWA NA UHABA WA WATAALAMU!


HOSPITALI ya Wilaya ya Korogwe Magunga inakabiliwa na upungufu mkubwa wa wataalamu wa fani ya uuguzi hali inayowalazimu watumishi hao kufanya kazi nzito kuliko uwezo wao.

Hadi sasa Hospitali hiyo ya Magunga ina jumla ya watumishi 153 ambapo kati yake ni 52 tu ndio wenye taaluma ya uuguzi huku wengine 101 wakiwa hawana taaluma lakini wanaendelea kutoa huduma katika hospitali hiyo.

Akizungumza na Blog hii Hospitalini hapo,Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Dakta Rashidi Saidi amesema hali hiyo inachangia kukwamisha juhudi za Hospitali hiyo kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Amesema tangu Hospitali hiyo ianze kutoa huduma mwaka 1952 hadi sasa inawahudumu 52 tu ambao walio ndio wenye taaluma hiyo kuku idadi kubwa wakiwa hawana taaluma.

Ameiomba Serikali kuiwezesha Hospitali hiyo kupata wataalamu wengi wa sekta hiyo ya Afya ili kuboresha huduma za kitabibu katika hospitali hiyo ambayo inategemewa na wakazi wengi wa wilaya ya Korogwe na Handeni.


Na Benedict Kaguo, Korogwe

No comments:

Post a Comment