BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, October 8, 2010

MKINGA YAISIFU TUMAINI ENVIRONMENTAL CONSERVATION GROUP!


HALMASHAURI ya wilaya ya Mkinga imesifu jitihada zinazofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Tumaini Environmental Conservation Group TECG lenye makao yake Kisosora jijini Tanga kwa juhudi za kuelimisha jamii juu ya uharibu wa mazingira ya bahari na Pwani.

Akifungua mafunzo ya athari za uharibifu wa mazingira ya bahari na Pwani yaliyohusisha Kata Tatu za wilaya ya Mkinga,Afisa Kilimo,Ushirika,Uvuvi wilayani Mkinga Dikta Benadetha Mwawado amesema serikali wilayani humo itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na shirika hilo kunusuru mazingira.

Dokta Mwawado amesema jukumu la kutunza na kuhifadhi mazingira ya bahari na Pwani ni la kila mwanajamii hivyo ni vema jamii ikaelimika na kujiepusha na vitendo vya uharibifu huo hasa uvuvi haramu.

Mafunzo hayo yamewahusisha wavuvu,maafisa watendaji na vijiji na Maofisa Uvuvi wa Wilaya hiyo na kutolewa na Shirika hilo la TECG kwa ufadhili wa mfuko wa hifadhi ya mazingira ulimwenguni WWF

No comments:

Post a Comment