BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, October 18, 2010

VIGOGO WA CCM TANGA WABWAGA MANYANGA!!

Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tanga kimepata pigo baada ya viongozi wake mashuhuri kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kwa kile walichodai ni baadhi ta wanachama kukosa imani dhidi yao. Wanachama hao waliandika barua za kujiuzulu nafasi zao huku wengine wakihama kabisa chama na kujiunga na Chama cha Wananchi CUF na kusababisha mgawanyiko mkubwa katika chama hicho.

Katika barua yake ilioandikwa kwa Katibu wa UVCCM wilaya ya Tanga ambayo Blog hii inayo nakala yake Kigogo wa Chama hicho Kata ya Ngamiani Kati Bi.Fatihiya Nyalusi alitangaza rasmi kujiuzulu nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani Chama.

Nyalusi ambaye alikuwa ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Ngamiani Kati huku akiwa Katibu wa Uhamasishaji wa Kata hiyo kupitia Jumuiya ya Vijana (UVCCM). Mbali na Nyalusi wengine waliotangaza kujiengua katika Chama hicho ni aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Tanga Hassan Omari ambaye pia ni alikuwa kiongozi wa Tawi A katika Ngamiani kati tawi A.

Omari ambaye alitangaza kujitoa CCM na kujiunga na CUF wakati mgombea Urais wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipofanya mkutano wake katika uwanja wa Tangamano. Kujiengua kwa viongozi hao mashuhuri katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu kimetasfiriwa na wachambuzi wa siasa za Tanga kuwa huenda ukaongeza mpasuko uliopo kwa sasa na kuhatarisha ushindi wa CCM katika nafasi za Udiwani na Ubunge.

Katika barua yake ya Oktoba 4 mwaka huu ambayo Blog hii inayo nakala yake, Nyalusi alisema ameamua kujiuzulu kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kifamilia na vilevile viongozi wa Chama kukosa imani naye. “Kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kifamilia na vilevile uongozi wa Chama kukosa imani na mimi nitakuwa mwanachama wa CCM” ilisema sehemu ya barua hiyo.


Na Oscar Assenga,Tanga

No comments:

Post a Comment