BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, October 21, 2010

HISTORIA YA MUZIKI WA TAARAB KUTOKA TANGA!

(Pichani Waziri Ally wa Kilimanjaro Band, wakati huo akiwa Lucky Star akipiga kinanda)

Katika miaka ya 50 wanawake tisa wa Tanga walijikusanya na kuanzisha wakaanzisha kikundi cha kuimba walichokiita Raha til Fuad maana yake Raha ya Moyo. Akina mama hawa chini ya bibie aliyeitwa Mama Akida au aka Mama Lodi, waliendesha kikundi chao wakiwa wanaimba nyimbo za Siti Binti Sadi na tungo zao ambazo waliimba katika melody ya nyimbo za kihindi zilizotamba wakati huo.

Kundi hili liliendelea na kuanza kuruhusu wanaume kujiunga hasa wakiwa wapiga vyombo. Hata mtoto wa Mama Akida, Akida Jumbe hatimaye alijiunga na kundi hili kama mpiga accordion kwenye mwaka 1962. Kundi hili ambalo baadae lilikuja kuitwa Young Noverty,liliendelea mpaka kukaweko na mgawanyiko uliozaa kundi la Shaabab Al Waatan. Hapa ndipo kukaanza mtindo wa kuweko kundi pinzani jambo ambalo kwa njia ya ajabu sana limekuwa linadumu kiasi cha miaka kumi kumi.

Miaka ya 1960s Young Noverty na Shabaab al Waatan, 1970s Lucky Star Musical Club na Black Star Musical Club, 1980 Golden Star Taarab na White Star Taarab, 1990, Babloom Modern Taarab na Freedom Modern Taarab. Taarab ya Tanga ndo haswa inastahili kuitwa modern Taarab, kwani wao hawkufuata taarab ile iliyoletwa Zanzibar enzi ya Sultan Seyyid Barghash, kundi la taarab hii lilikuwa dogo na vyombo vyake vilikuwa pamoja na Gitaa la besi, gitaa la solo, drums bongos ,akodion au kinanda.

Nyimbo zao zilikuwa fupi na si ndefu kama za Kizanzibari., nyimbo zilitegemea mipigo ya ngoma za asili za kumbwaya na chakacha na hata baadaye mitindo kama rumba,bossa nova ilitumika kama mapigo. Na Taarab ya Tanga ndio iliyoanzisha moto wa vikundi vya taarab Tanzania Bara.

Moshi kulikuwa na New Alwatan,AzimioTaarab, na Blue Star Taarab , Arusha-Blue Star Taarab,Dodoma-Dodoma Stars,Kondoa –Blue Stars,Mbeya-Magereza Kiwira, Mwanza-ujamaa Taarab, Bukoba –Bukoba Stars, na muendelezo huu uliingia mpaka Burundi kutokana na mwana muziki mmoja alie julikana kama Athmani Mkongo, alitoka Burundi na bendi yake kufika Tanga akawa mwanamuziki mahiri wa Taarab na hata kuipeleka kwao Burundi.

No comments:

Post a Comment