MGOMBEA Mwenza wa Nafasi ya Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM,Dakta Mohamed Gharib Bilal amesema tatizo la upungufu wa nyumba za walimu hapa nchini litakuwa historia ikiwa wananchi watakipa ridhaa chama hicho kushika dola Oktoba 31 mwaka huu.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga kwenye mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tangamano jijini Tanga jioni ya jana,Dokta Bilal amesema tatizo la nyumba za walimu linazozikabili shule nyingi za sekondari za kata hapa nchini litamalizika ikiwa wananchi watakichagua chama hicho.
Amesema jumla ya Shilingi Bilioni 250 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu ili kuwawezesha walimu kupata makazi bora hasa kwenye sekondari za Kata.
Kuhusu Afya Dokta Bilal amesema Hospitali za Mikoa zilizopo hapa nchini ikiwemo hospitali ya Bombo zitageuzwa hospitali za rufaa ili kuzipunguzia mzigo wa utoaji huduma unaozikamili kwa sasa.
Hata hivyo Dokta Bilal amesema Serikali ijayo itahakikisha inaboresha maisha ya watanzania kwa kujenga uchumi imara ili ifikapo mwaka 2025 Tanzania iweze kuwa kama nchi za Singapore na Malaysia.
Mgombea Mwenza huyo wa Urais wa Tanzania ameanza jan ziara yake ya Kampeni Mkoani Tanga akitokea Mkoa wa Pwani ambapo akiwa Pangani alimnadi Mgombea ubunge wa jimbo hilo Salehe Pamba ambapo na hapa jijini Tanga alimnadi Bw.Omari Nundu
Na Benedict Kaguo, Tanga
No comments:
Post a Comment