BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, October 18, 2010

SALAM KUTOKA DENMARK!!

Tanga ya Mjarumani, ni mji wa kizamani aliovutiwa mkoloni na hatimae kukaa hapa nchini. Wa mbali na mikoani, walikuja mashambani, sikwambii viwandani na pirika za bandarini. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Umaarufu Mwambao, kwenye bahari ya Hindi umeandikwa ubao, kuwa siku hazigandi, Elimu ndio ufunguo, idai japo hupendi, jamani muhimu ngao, ndio siri ya ushindi Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Inakupenza imani, na hiyo yako subira, umeanikwa juani, kwa kupenda hadhara Tanga umaskini, na hali wewe ni bora amka upo vitani, kabla hujawa ngawira. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Umekuwa Tanga bora, kwa kutaka yako kura, nawe usifanye papara ukaipata hasara bila uwape harara, natumbo lenye kuhara silaha yako ni kura, mpe kiongozi bora. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Kushindwa kulinda maji, chura na chake kijicho amkeni wana mji, fungueni yenu macho sasani wenu mtaji, mtapata mtakacho danganya kuitwa jiji, wacheza mwanjificho. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??


Shairi hili nimetumiwa na mdau wa Vijimambo Vya Tanga kutoka Copenhagen, Denmark.

No comments:

Post a Comment