BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, October 4, 2010

DC HANDENI AHIMIZA UJENZI WA MADARASA!


WAZAZI wilayani Handeni Mkoani Tanga wamehimizwa kuelekeza nguvu zao katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari na nyumba za walimu ili kuwawezesha wanafunzi wote watakaofaulu kujiunga na Sekondari waweze kupata nafasi hiyo.

Akizungumza na Blog hii ,Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Kapteni Mstaafu Seif Mpembenwe alisema kwa sasa kazi inayoendelea wilayani humo ni kuelimisha wananchi ili waweze kujenga madarasa hayo ili kutoa fursa kwa watoto wao kupata elimu.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa sasa inakwenda vizuri ambapo asilimia 60 ya madarasa yameshakamilika yakisubiri wanafunzi.

Alisifu juhudi za wazazi hao ambao wamekuwa wakiitikia wito wa kujenga vyumba vya madarasa kwani kwa kufanya hivyo watawezesha wanafunzi wengi zaidi kujiunga na sekondari na kukabiliana na adui ujinga.

Aliwataka wazazi hao kuongeza nguvu katika ujenzi wa nyumba za walimu ili kuwavutia zaidi walimu kufanya kazi katika wilaya hiyo hasa vijijini

Alisema kuwa wanafunzi wote watakaofaulu kujiunga na sekondari ni lazima waingie kidato cha kwanza hivyo wazazi hawana budi kujizatiti katika kuhakikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa unafanyika mapema.

“Tunashukuru kasi ni nzuri na kwamba wanafunzi watakaofaulu wataenda Sekondari,wazazi tunashirikiana nao vizuri kwenye ujenzi wa madarasa”alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

No comments:

Post a Comment