BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, October 22, 2010

PANGANI WAIKASIRIKIA CCM KUHUSU HIFADHI YA SAADAN


WANANCHI Wilayani hapa wameishutumu Serikali kwa kuhamishia Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani kutoka Mkwaja na kuyapeleka Bagamaoyo na kudai hizo ni njama za kudhoofisha uchumi wa Pangani.

Waliahidi kumchagua mgombea ambaye atakuwa na ushupavu wa kuyarejesha makao hayo makuu kuwa Pangani kama awali kwa kuwa ndiyo yenye eneo kubwa la hifadhi hiyo ambayo ni asilimia 75 kuliko upande wa Bagamaoyo.

Walitoa shutuma hizo hivi karibuni wakati wakiuliza maswali kwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Pangani kupitia CUF, Omar Ali Mohamed (Masomaso) katika mdahalo uliofanyika ukumbi wa Safari Annex mjini hapa.

Hoja hiyo ilianzishwa na mwanajopo katika mdahalo huo,Aweso Jabu ambaye alimhoji mgombea huyo kama anafahamu kuwa Serikali imehamisha makao makuu ya Hifadhi ya Saadani kutoka Mkwaja kuipeleka sehemu ya Bagamoyo.

Licha ya mwezeshaji wa mdahalo huo Lilian Kallaghe kuwataka washiriki wa mdahalo huo kutorudia maswali yaliyoulizwa, lakini karibu kila aliyekuwa akisimama aliweza kugusia kuhusu mbuga hiyo huku wakilalamika kuwa kuna ajenda ya siri ya kuhujumu uchumi wa Pangani.

Akijibu swali hilo, Mgombea huyo wa CUF ambaye ndiye pekee aliyejitokeza katika mdahalo huo, alieleza kukerwa na kitendo hicho na kusisitiza kuwa iwapo atachaguliwa atahakikisha Makao makuu ya Saadan yanarejeshwa Pangani.

No comments:

Post a Comment