BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, September 24, 2010

NIMR TANGA YATIMIZA MIAKA 30!

Mkuu wa mkoa wa Tanga Said Said Kalembo amesema kuwa magonjwa mengi yanayoikabili Tanzania yanahitaji mchango wa Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binaadamu NIMR katika kutafuta ufumbuzi wake pia amewasihi kupanua shughuli zao za utafiti kwa kuhusisha maeneo mengi yenye kipaumbele ukiacha malaria na utafiti wa virusi vya ukimwi pekee.

Ameyasema hayo wakati wa maonesho ya hadhara ya utafiti yanayojulikana kama OPEN DAY ya taasisi hiyo ya NIMR katika kituo chake kilichopo Mkabara na hospitali ya mkoa ya bombo mkoani Tanga hapo jana ikiwa ni maandalizi ya kutimiza miaka 30 yatakayofanyika 0ktoba mwaka tangu kuanzishwa kwake.

Aidha ameongeza kuwa NIMR mkoani hapa imebeba jukumu kubwa katika vituo malumu viavyotumika kufuatilia uwezo wa dawa za kutibu malaria na imefanya kazi na taasisi nyingine kwa karibu kutoa takwimu kwa wizara ya sfya na usitawi wa jamii kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti malaria (NMCP).

Ameongeza kuwa takwimu zilizopatiakana zilikuwa muhimu katika kufanya mabadiliko ya sera ya tiba ya malaria Tanzania ,na kuamini kuwa takwimu nyingi zitatolewa kwa kufuatilia dawa ya awali inayotumika kutibu malaria kwa sasa yaani ALU na nyinginezo.

Maabara hii pia inatoa msaada kwa program nyingine kama NLFP ambayo kiwango kilichopo kwa kutokomeza ugonjwa wa matende na mabusha hupimwa kwenye mbu kwa kutumia utalamu wa PCR ,aidha wataalamu wa maabara wa AMBRELA wanashiriki kupima malaria kimataifa kwa ajili ya kuangalia kiwango chao cha ubora katika kupima malaria kwenye utafiti ya chanjo ya RTS,S unaoendelea wilayani Korogwe.No comments:

Post a Comment