BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, September 21, 2010

DEEP SEA KWA CHINI LEO ASUBUHI!!

Taa ni moja ya kiumbe cha baharini. Hutumika kitoweo kama walivyo samaki wengine. Hapa akiwa ametoka kuvuliwa muda mchache tu....Taa hupatikana kwa wingi sana eneo la Deep Sea ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa samaki kwa jumla na reja reja hapa jijini Tanga.

Akiandaliwa, tayari kwa kukatwa vipande vipande auzwe!

Upande mwengine...kijana huyu nilimkuta akimkata kata samaki wa mteja aliyeomba amuandae ili kuepusha usumbufu pindi atakapofika nyumbani. Vijana wengi eneo hili wameamua kujiajiri wenyewe kwa kazi hiyo. Hutoza mteja kwa bei ya 500/=

Samaki punde wanapotoka kwenye ngalawa...hupangwa kwenye meza na kuuzwa.

Kwa mbali watu wakisubiri ngalawa kutia nanga ili wapate kitoweo cha samaki.

Ukiwa Deep Sea kwa chini, kila mtu yupo makini kutazama ni ngalawa gani inaingia ili kuwahi samaki wazuri kwa ajili ya biashara zao huko mtaani.No comments:

Post a Comment