SERIKALI imesifu juhudi kubwa zinazofanywa na Mashirika ya yasiyo ya kiserikali (Ngo’s) Mkoani Tanga katika kusukuma kwa kasi maendeleo ya wananchi hapa nchini.
Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Taifa ya Uratibu wa mashirika yasiyokuwa ya Serikali kilichofanyika jijini Tanga, Makamu Mwenyekiti Bodi hiyo Bw.Elichim Simpasa alisema Mashirika hayo yamesaidia kuharakisha maendeleo katika jamii kwenye nyanja mbalimbali hasa elimu, afya na mazingira.
Bw.Simpasa alisema licha ya changamoto zinazozikabili Asasi hizo lakini bado zimekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa kwani kazi zinazofanywa na mashirika hayo zilipaswa kufanywa na Serikali. “Tunatambua Ngo’s nyingi zinafanya kazi nzuri ya kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali kama elimu,afya na mazingira,tunaomba muendelee na moyo huo ili kuweza kuijenga jamii iliyobora”alisema Bw.Simpasa
Kikao hicho ambacho kilishirikisha washiriki 67 kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi mkoani Tanga kiliwawezesha kutambua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mambo yanayosimamiwa na bodi hiyo pamoja na suala la usajili wa Ngo’s hapa nchini
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Asasi ya TOWOREC,Bi.Anna Manento na Mkurugenzi wa Tayodea Bw.David Chanyegea wamesifu juhudi zinazofanywa na bodi hiyo katika kuwakunatisha pamoja kujadili maendeleo na changamoto za asasi hizo zisizo za kiserikali.
Na Benedict Kaguo,Tanga.
No comments:
Post a Comment