BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, September 6, 2010

PROF. MAJIMAREFU AVUNJA NGOME ZA CUF KOROGWE VIJIJINI

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Majimarefu ameendeleea 'kuua' upinzani wilayani hapa baada ya wanachama wa CUF 41 kuhama chama hicho na kujiunga na CCM.

Wanachama hao walijiunga mwishoni mwa wiki kwenye mikutano ya kampeni ya Bw. Majimarefu kwenye kata za Mpale na Bungu, huku akizifunga kabisa ofisi za CUF tawi la Kwemshai kata ya Bungu baada ya viongozi wake na wanachama 28 kuhamia CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari aliekuwa Katibu wa CUF Tawi la Kwemshai Bw. Hamdani Sakota alisema wameamua kujiunga CCM baada ya kuwa na matumaini na Bw. Majimarefu, kwani anaweza kutatua kero zao.

"Sisi watu wa tarafa ya Bungu tuna kero mbalimbali kama barabara na maji, lakini kwa Majimarefu kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM Jimbo la Korogwe Vijijini atatusaidia hata kutufanyia ukarabati nyumba za ibada misikiti na makanisa" alisema Bw. Sokota.

Wanachama wengine 13 walijiunga CCM wakitokea CUF kwenye kata ya Mpale, huku wakijinasibu kuwa matatizo yao yamepata mtatuzi ambaye ni Bw. Majimarefu.

Naye Bw. Majimarefu akizungumza na waandishi wa habari alisema wameanzisha operesheni ya kuhakikisha wanakijenga chama kwa kuingiza wanachama wengi CCM, lakini pia sera zao za kuboresha maisha ya Watanzania zinatekelezeka.

"Tumejipanga kuona tunapata ushindi kwa kishindo Jimbo la Korogwe Vijijini, lakini pia ili kushinda unatakiwa kuwavuta wananchi wengi, hivyo tutazidi kuchukua wanachama wengi kutoka upinzani" alisema Bw. Majimarefu.


NA Sussan Uhinga, Korogwe Vijijini

No comments:

Post a Comment