BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, September 2, 2010

TUTAENDELEA KUZUNGUMZA UDHAIFU WA CCM- YASEMA CHADEMA!

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,kimesema kitaendelea kuzungumza udhaifu wa Serikali ya chama cha Mapinduzi kadiri watakavyokuwa wanapata nafasi ya kufanya hivyo. Mbali na udhaifu pia Chama hicho kimesema kitapongeza mafanikio ya baadhi ya maeneo kama wananchi watakuwa wayaona.

Mwenyekiti wa CHADEMA, wilaya ya Tanga,Bw.Mohamed Kinomi alisema hayo wakati wa mkutano wao wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni ya kumnadi mgombea ubunge wa Chama hicho, Bw.Kassim Amari uliofanyika barabarara ya 14 jijini Tanga.

Alisema huwezi kuzungumzia udhaifu uliopo katika mambo mbalimbali bila kukitaja Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kilichopewa dhamana ya kuongoza tangu nchi ilipopata uhuru.

“Lazima utabidi ufike wakati tuhoji utendaji wa CCM na Serikali yake katika kipindi chote tangu nchi ilipopata uhuru imefanya nini katika kuwakomboa wananchi wake”alisema Bw.Kinomi.

Awali mgombea ubunge wa CHADEMA Bw.Amari aliwaomba wananchi wa Tanga kumchagua kwani yeye ni kijana na anafahamu shida zote za vijana hasa tatizo la ukosefu wa ajira kwa kuishinikiza Serikali ifufue viwanda vilivyokufa Tanga.

Na Benedict Kaguo,Tanga

No comments:

Post a Comment