BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, September 13, 2010

BREAKING NEWS!!!! DR LEADER AJITOA MOTIKA RECORDS!!!Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwenda kwa jina la "Macho Kodokodo" Lucas Silas a.k.a Dr.Leader" ameeleza kuwa sababu za kujitoa katika lebo ya Motika Production kutokana na kutokuwa na maslahi ya kutosha katika lebo hiyo ambayo inamilikiwa na msanii wa muziki huo hapa nchini Mr.Ebbo.

Akizungumza na Blog hii msanii huyo ambaye kwa sasa yupo mbioni kukamilsha ujio wa video yake mpya ya wimbo wa 'Kagoma Kwenda' alisema kuwa kuondoka kwake ni kutokana na kufanya kazi bila kuona mafanikio yake kwa wakati hali iliyo mpelekea kuuona mziki kuwa mgumu kwa upande wake.

Msanii huyo pia amekanusha uvumi uliojitokeza hivi karibuni kuwa alimkimbia Mr.Ebbo na kusema kuwa haikuwa kweli bali yale yalikuwa ni makubaliano yake mkataba aliokuwa nao na Motika Production ulikuwa ni kufanya album moja na kuendelea na mambo mengine. "Kwa sasa ninachokiangalia ni jinsi gani nitafanya kazi nzuri na yenye kuvutia kwa mashabiki wangu ambao kwa sasa watakuwa na kiu ya kutaka kusikia Dr.Leader anafanya nini " alisema Msanii huyo.

Aidha alisema kuwa kwa sasa anatarajiwa kufanya kazi mbalimbali nzuri ambazo zitamfanya aweze kutambulika kitaifa na kimataifa katika anga za muziki wa kizazi kipya hapa nchini na kuweza kuiletea heshima mkoa wa Tanga na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment