IDADI ya watalii wa ndani wanaotembelea vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Pangani Mkoani Tanga imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka hivyo kuongeza pato litokanalo na sekta ya Utalii wilayani humo.Ongezeko hilo la watalii wa ndani kutembelea vivutio hivyo vya watalii linatokana na juhudi zinazofanywa na Serikali na wadau mbalimbali katika kuhamasisha utalii wa ndani hapa nchini.
Akizungumza na Blog hii Mratibu wa Kituo cha kuendeleza Utalii cha Pangani coast cultural tourism program Bwana Leonard Sekibaha amesema watalii hao wanazidi kuongeza mwaka hadi mwaka kutokana na elimu ya kutembelea vivutio hivyo kuendelea kuwafikia wananchi walio wengi. Amesema tangu mwezi Januari hadi June mwaka huu watalii hao wamefikia 149 ikilinganishwa na watalii 22 waliokuwa wamefika katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka juzi.
Amesema katika kipindi hicho cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka jana watalii hao wa ndani wamefikia 52 na kuongeza kuwa idadi hiyo kwa sasa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.Amewahimiza wananchi Mkoani Tanga kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyopo wilaya humo ili kujifunza na kujionea fursa mbalimbali zinazoweza kuwaondoa wananchi katika wimbi la umasikini.
No comments:
Post a Comment