MUUNGANO wa wasafirishaji Tanga (MUWATA) umelalamikia kuendelea kupanda kwa kasi bei ya mafuta huku kiwango cha nauli kilichopangwa na SUMATRA kikipaki kuwa pale pale.
Kaimu Mwenyekiti wa MUWATA Bwana Hatabwi Shaaban amesema kwa sasa bei ya mafuta imepanda hadi kufikia Shilingi 1700 kwa lita huku kiwango cha nauli kikisalia kile kile kilichopangwa hapo awali.
Amesema nauli hiyo kwa sasa Shilingi mia tatu hadi mwisho wa ruti lakini baadhi ya abiria wamekuwa wakiomba Shilingi 200 kutokana hali duni ya kiuchumi.
Wameimba serikali kupitia ewura kuweka udhibiti wa bei ya nishati ili kupunguza kupanda holela gharama kwani inaathiri uendeshaji wa shughuli za usafirishaji jijini Tanga.
Amesema wakati nauli hizo zinapangwa lita moja ya mafuta ilikuwa ni shilingi 1250-1300. Akizungumzia malalamiko hayo Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Mkoa wa Tanga Bwana Johns Makwale,amesema viwango vya nauli vinavyopangwa vinaangalia vigezo zaidi ya kumi,huku suala la mafuta likiwa ni moja wapo.
Hata amesema kama kweli kuna haja ya kubadili kiwango cha nauli kuna utaratibu wa kufuatwa kwa ili kuangalia uwezekano wa kubadili kiwango hicho.
Na Benedict Kaguo, Tanga
No comments:
Post a Comment