BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, September 20, 2010

JESHI LA POLISI TANGA LAWAMANI!!!

(Kituo cha polisi Chumgbageni kwa mbaali katika picha!)

JESHI la polisi mkoani hapa limeingia lawamani kufuatia mahabusu ya Chumbageni kudaiwa kuwa chafu ambapo mahabusu wamekuwa wakiishi kwenye maji taka, kukosa hewa safi jambo ambalo limekuwa likihatarisha maisha yao kwa vile miundombinu ya awali imebadilishwa ujenzi wake.

Watu ambao waliwahi kukumbwa na makosa mbalimbali hali iliyowalizimu kuwekwa kwenye mahabusu hiyo wameliambia Blog hii kwamba hali ilivyo sasa kwenye mahabusu hiyo sio shwari na inahatarisha maisha ya binadamu kwa vile wanaishi kwenye uchafu uliozagaa eneo lote la ndani.

Licha ya hilo walisema kwamba hewa wanayovuta kwa sasa ni ile chafu kwa vile unapoingia ndani ya mahabusu huwezi kuvuta hewa kama zamani kwa vile ujenzi wa awali tokea enzi la utawala wa mkoloni umebadilishwa ambapo sasa kumewekwa matundu madogo ya kutolea hewa na kuingiza mwanga.

“Sote ni mahabusu watarajiwa, sio wote wanaoingizwa kule wanamakosa lakini utashangaa ujenzi wa utawala wa kikoloni wa vyuma umebadilishwa na sasa kumewekwa matundu madogo tu jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya watu ambapo pia kuna mlundikano mkubwa wa mahabusu” alisema Kenedy.

Kuhusu suala la maji machafu kutoka chooni kutiririka muda wote sehemu wanazoishi mahabusu hao Kenedy ambaye aliambatanana mwenzake Juma walisema kwamba inatokana na vyoo kufurika uchafu huku mabomba ya maji yakiwa mabovu jambo ambalo limesababisha maji hayo kutoka muda wote.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii kuhusiana na habari hizo kamanda wa polisi mkoani Tanga Liberatus Sabasi alikana kubadilishwa kwa ujenzi wa miundombinu ndani ya mahabusu hiyo na kwamba madirisha hayo yako kwa ajili ya usalama ambapo watuhumiwa hawatakiwi kupanga mbinu.

Pia alisema tatizo la kumwagika kwa maji taka ndani ya mahabusu hiyo alisema, linatokana na baadhi ya mahabusu kuharibu miundombinu hiyo mara kwa mara huku akieleza kwamba jeshi la p[olisi limekuwa likijitajihidi kuifanyia matengenezo mara tu inapoharibika ili kuweka usafi wa mazingira vizuri.

“Ndugu mwandishi nakuhakikishia mahabusu ni safi tena ni ya kisasa yenye kukidhi viwango na leo nimetoka kutembelea huko, kuhusiana na maji machafu huwa tunatumia ndoo OCD huwa anawapelekea ndoo ili kuhifadhia uchafu hivyo hali sio kama inavyoelezwa” alisema Kamanda Sabasi.

Vilevile Kamanda Sabasi alieleza kwamba mahabusu ya wanawake imejengwa kisasa ambapo imeweza kukidhi viwango na iko katika hali ya usafi na ndio ambayo imejengwa katika siku za hivi karibuni na kudai kuwa yanayozungumzwa ni uzushi mtupu na hayana ukweli wowote kwa wakati huu.

Akizungumzia tatizo la msongamano wa mahabusu kamanda Sabasi alisema hali hiyo inatokana na ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia mahabusu katika mahakama ambapo mahabusu wa muda mrefu wakati mwingine hulazimika kuhifadhiwa kwenye kituo hicho cha polisi cha Chumbageni jijini Tanga.

Na Sussan Uhinga,Tanga.

No comments:

Post a Comment