BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, September 15, 2010

"UJIO WANGU MPYA BAADA YA BINADAMU"- ASEMA UNTOUCHABLE


(Untouchable akiwa na Matonya studio)

Msanii nguli wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania anayetokea Tanga Wilson Lusingu a.k.a Untouchable, anatarajia kuachia ngoma yake nyengine baada ya 'BINADAMU' aliyomshirikisha Kassim kufanya vizuri katika game ya muziki wa Bongo Flava.

Akizungumza na Blog hii Untouchable amesema kuwa, ngoma hiyo mpya bado hajaipa jina...."kiukweli ngoma imeandikwa na inazungumzia maisha sasa jina kamili kiukweli ngoma haijapewa ikikamilika ndiyo jina litajulikana kama ilivyokuwa kwa Binadamu bro" Alisema msanii huyo.

(Untouchable akiwa na Dully)

Aidha Untouchable aliongeza kuwa ngoma hiyo bado haijakamilika kutokana na msanii ambae amempa shavu katika ngoma hiyo "Matonya" kutoonyesha ushirikiano wa kutosha katika kumalizia wimbo huo ambao anaufanyia pale AM Records kwa Maneke!

Unaweza kusikilia 'Binadamu' Hapo juu pembeni palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Upo kwenye List, wimbo namba tisa!


No comments:

Post a Comment