BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, September 16, 2010

BANDARI MPYA TANGA KUANZA KUJENGWA MWAKA 2018

MRADI wa ujenzi wa bandari mpya eneo la Mwambani jijini Tanga unatarajiwa kuanza utekelezaji wake mwaka 2018 baada ya kukamilika tathmini iliyofanywa na Benki ya Dunia. Bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia shehena milioni 3.88 za makontena mchanganyiko kwa mwaka ikiwa ni maoni ya wataalamu washauri wa mradi huo.

Meneja wa Bandari ya Tanga, Zakaria Misso alisema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya bandari hiyo kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika jijini hapa.

Alisema katika kutekeleza mradi huo, tayari ekari 92.8 za ardhi zimetwaliwa na mamlaka hiyo ambapo wakazi wa eneo hilo tayari wameshalipwa fidia kupisha ujenzi huo wa bandari mpya.

Hata hivyo, eneo hilo la ekari 92.8 limeonekana kutokidhi mahitaji ya bandari hiyo ambapo inahitaji ekari nyingine 82 kutoka Halmashauri ya Jiji ili kutekeleza mradi huo ambapo jumla ya sh bilioni 2.1 zinahitajika kulipa fidia wakazi hao.

No comments:

Post a Comment