BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, September 30, 2010

PROF. MAJI MAREFU AMPA NG'OMBE MAMA SALMA KIKWETE!

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Korogwe vijijini Steven Ngonyani Profesa Maji Marefu amempatia zawadi ya ng’ombe mke wa Rais Mama Salma Kikwete kama zawadi ya kuhimiza ufugaji ili kutekeleza Kilimo Kwanza.

Mgombea huyo ubunge ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuwa karibu na wananchi na kujishughulisha na kazi za kilimo na ufugaji pamoja na utaalamu wa tiba za asili.

Alisema zawadi hiyo imelenga kumwezesha Mama Salma kufanya kazi ya ufugaji ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya Kilimo kwanza kinachosisitiza juu ya kilimo na ufugaji wa kisasa.

Akipokea zawadi hiyo Mke Rais Mama Salma alimshukuru Profesa Maji Marefu kwa zawadi hiyo na kusema kuwa itamsaidia kuongeza zizi lake kwa kufuga ngombe zaidi.

Alisema zawadi hiyo ya ngo’mbe dume itamuwezesha kuongeza ufanisi katika ufugaji wa ngombe ili kujiongezea kipato kupitia ufugaji..

Na Benedict Kaguo, Korogwe.

SERIKALI YASIFU MCHANGO WA NGO'S TANGA!


SERIKALI imesifu juhudi kubwa zinazofanywa na Mashirika ya yasiyo ya kiserikali (Ngo’s) Mkoani Tanga katika kusukuma kwa kasi maendeleo ya wananchi hapa nchini.

Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Taifa ya Uratibu wa mashirika yasiyokuwa ya Serikali kilichofanyika jijini Tanga, Makamu Mwenyekiti Bodi hiyo Bw.Elichim Simpasa alisema Mashirika hayo yamesaidia kuharakisha maendeleo katika jamii kwenye nyanja mbalimbali hasa elimu, afya na mazingira.

Bw.Simpasa alisema licha ya changamoto zinazozikabili Asasi hizo lakini bado zimekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa kwani kazi zinazofanywa na mashirika hayo zilipaswa kufanywa na Serikali. “Tunatambua Ngo’s nyingi zinafanya kazi nzuri ya kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali kama elimu,afya na mazingira,tunaomba muendelee na moyo huo ili kuweza kuijenga jamii iliyobora”alisema Bw.Simpasa

Kikao hicho ambacho kilishirikisha washiriki 67 kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi mkoani Tanga kiliwawezesha kutambua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mambo yanayosimamiwa na bodi hiyo pamoja na suala la usajili wa Ngo’s hapa nchini

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Asasi ya TOWOREC,Bi.Anna Manento na Mkurugenzi wa Tayodea Bw.David Chanyegea wamesifu juhudi zinazofanywa na bodi hiyo katika kuwakunatisha pamoja kujadili maendeleo na changamoto za asasi hizo zisizo za kiserikali.

Na Benedict Kaguo,Tanga.

MADEREVA WA PIKIPIKI WAANDAMANA MUHEZA!


WAENDESHA pikipiki za bodaboda wapatao zaidi ya 50 wameandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mathew Nasei wakidai mwenzao amepigwa na askari polisi na kuwekwa mahabusu.

Tukio hilo la kuandamana vijana hao lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi wakiwa na pikipiki zao huku wakiwa wanapiga honi na kuimba.

Vijana hao baada ya kufika katika ofisi za mkuu wa wilaya walimuona na kumueleza kwamba kuna mwenzao amepigwa na polisi na kuwekwa mahabusu kwa madai amekaidi amri ya polisi.

Mmoja ya vijana hao wa bodaboda , Selemani Juma akizungumza na mkuu wa wilaya kwa niaba ya wenzake, alisema polisi walifika maeneo ya kituo cha mafuta cha BP na kumkuta dereva wa pikipiki ya bodaboda amekaa juu ya pikipiki yake huku ikiwa imeiegesha.

Alisema polisi hao walimhoji kijana huyo aliyekuwa amekaa katika pikipiki yake kuwa aonyeshe leseni yake na kofia ya pikipiki.

Juma alisema kuwa kijana huyo aliwajibu polisi kwamba hana kofia aliiacha kwa sababu haendeshi pikipiki bali alikaa juu ya pikipiki hiyo.

Alisema baada ya kijana huyo aliyekuwa amekaa katika pikipiki hiyo kujibu hivyo, polisi walianza kumpiga wakidai aliwaletea jeuri wakiwa kazini na kumpeleka mahabusu katika kituo cha polisi.

Hata hivyo akijibu malalamiko hayo mkuu wa wilaya alisema kuwa tatizo lao atalishughulikia baada ya kuzungumza na upande wa pili yaani polisi, lakini hawezi kusikiliza upande mmoja.

Alisema kuwa yeye anajukumu kubwa la kutetea wananchi, lakini akasema kuwa waendesha pikipiki za bodaboda wamekuwa na tabia ya kuvunja sheria ya kukaidi kuvaa kofia pamoja na kwenda mwendo wa kasi.

Na Steven William, Muheza

IFAHAMU REDIO HURUMA YA JIJINI TANGA!

Radio Huruma,Tanga Diocese Multimedia Company LTD (TDMCL) Box 1108 Tanga, Fax: 027-2643548, Phone: Office Hours 027-2645999, Mobile +255 784 469 051, +255 784 680 686, E-mail radiohuruma@gmail.com - Chumbageni - Pwani House.

BACKGROUND.NAME OF THE RADIO:
RADIO HURUMA (RH)

OWNER OF THE RADIO
TANGA DIOCESE MULTIMEDIA COMPANY LTD (TDMCL)
c/o THE CATHOLIC DIOCESE OF TANGA,
P.O. BOX 1108,
TANGA, TANZANIA

WHEN IT WAS STARTED
The Radio was officially opened on the 24th December 2007

BROADCASTING FREQUENCY
The Radio Huruma Broadcasts in FM BAND 103.6 MHz

MOTTO OF THE RADIO
‘FARAJA KWA JAMII’
BROADCASTING STUDIO
The Radio Huruma studio is at the Cathedral Church of Tanga, Chumbageni near the road to Mombassa Kenya.

The broadcasting house is called Pwani House.

MAIN TRANSMITTING TOWER.
The main transmitting tower is situated at Mkanyageni village near Muheza, it is about 25KM form the Main studio.

OBJECTIVES:
The main objective of Radio Huruma (RH) is to sensitize the people of Tanga Region on issues of Development and spread the word of God. The TBC Taifa before known as (Radio Tanzania Dar Es Salaam), highlights national issues. It is only once in a while that there is mention of Tanga community interests. With this deficit in mind, the Catholic Diocese of Tanga proposed to set up a Radio Station which will mainly focus on Tanga day to day activities and promote the social and economic well-being.

Radio Huruma always seeks to educate, inform, entertain and inspire the community in matters that promote peace, love and justice and while at the same impart the knowledge of God. And in so doing, complement the government in its effort to combat social evil and moral digression.

Radio Huruma strives in establishing a credible society with good conduct where the law is upheld.

Radio Huruma always aims at enhancing development by alleviating the shortcomings entailed in the fields of health, education, social services, justice, peace, care of the environment, natural resource, management, globalization ‘utandawazi’.

Radio Huruma helps the church, Catholic Diocese of Tanga, to fulfil its goal on providing service to the people of Tanga and Tanzania at large.

OUR COVERAGE:

1. TANGA Region

- Muheza district (all areas)
- Pangani district (all areas)
- Handeni district (all areas)
- Korogwe district (all areas)
- Mkinga district (all areas)
- Kilindi district (all areas)
- Lushoto district (some areas because of the geographical situation where Lushoto is a mountainous area).

2. Island of Pemba (all areas) pemba is very near to Tanga
3. Zanzibar (some areas)
4. Mombassa Kenya
5. Dar Es Salaam ( some areas found in the high land, especially outside the town)
6. Bagamoyo ( some areas)
7. Morogoro ( Kilosa, Mzinga the boarder of Morogoro and Dodoma, Kibaigwa)
8. Kibaha (some areas)
9. Kilimanjaro (some areas)Manyara (some areas)


Anything dont hesitate to ask through Program/Station Manager
cellphone +255 713 318561
email - rasodo56@gmail.com

Wednesday, September 29, 2010

TAYODEA YATOA SOMO LA UCHAGUZI MKUU 2010!


WANANCHI Mkoani Tanga wamehizwa kuchuja ahadi za wagombea zinazotolewa katika kipindi hiki cha Kampeni ili waweze kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo. Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana na Maendeleo Mkoani Tanga TAYODEA Bwana David Chanyegea wakati akizungumza na Blog hii katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Amesema hatma ya maendeleo kwa Mkoa wa Tanga yako mikononi mwao hivyo ni vema wakapima ahadi za wagombea na kuchagua viongozi bora bila ya shinikizo la mtu au kikundi fulani. Pia amewahimiza wananchi waliojiandikiasha kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaowataka.

Na Benedict Kaguo, Tanga.

WANAOVUMA KUTOKA TANGA!

Aliyevaa shati jeupe ni Dj Bob Nass wa redio Breeze Fm ya jijini Tanga, akiwa na msanii mahiri wa muziki wa Hip Hop nchini ambaye anatokea Tanga pia Wilson Lusing maarufu kama Untouchable.

MUWATA YAILALAMIKIA SUMATRA!


MUUNGANO wa wasafirishaji Tanga (MUWATA) umelalamikia kuendelea kupanda kwa kasi bei ya mafuta huku kiwango cha nauli kilichopangwa na SUMATRA kikipaki kuwa pale pale.

Kaimu Mwenyekiti wa MUWATA Bwana Hatabwi Shaaban amesema kwa sasa bei ya mafuta imepanda hadi kufikia Shilingi 1700 kwa lita huku kiwango cha nauli kikisalia kile kile kilichopangwa hapo awali.

Amesema nauli hiyo kwa sasa Shilingi mia tatu hadi mwisho wa ruti lakini baadhi ya abiria wamekuwa wakiomba Shilingi 200 kutokana hali duni ya kiuchumi.

Wameimba serikali kupitia ewura kuweka udhibiti wa bei ya nishati ili kupunguza kupanda holela gharama kwani inaathiri uendeshaji wa shughuli za usafirishaji jijini Tanga.

Amesema wakati nauli hizo zinapangwa lita moja ya mafuta ilikuwa ni shilingi 1250-1300. Akizungumzia malalamiko hayo Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Mkoa wa Tanga Bwana Johns Makwale,amesema viwango vya nauli vinavyopangwa vinaangalia vigezo zaidi ya kumi,huku suala la mafuta likiwa ni moja wapo.

Hata amesema kama kweli kuna haja ya kubadili kiwango cha nauli kuna utaratibu wa kufuatwa kwa ili kuangalia uwezekano wa kubadili kiwango hicho.

Na Benedict Kaguo, Tanga

AHMED KHATIBU- "WAWOOOOOO!!!!!"

Mtangazaji mahiri wa kituo cha redio cha Mwambao Fm jijini Tanga Ahmed Khatibu, akiwa katika pozz. Ahmed anatangaza kipindi cha Amka na Mwambao ambacho kinarushwa kila siku asubuhi, anatangaza pia Arabain Flava, Nyumba ya Mwafrika pamoja na kipindi cha Michezo. Mwambao Fm inapatikana katika masafa ya 106.6 ukiwa mkoani Tanga.

Tuesday, September 28, 2010

MATONYA KUPIGA SHOW LONDON!!


Msanii kutokea mkoani Tanga ambaye anafanya vizuri kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava nchini, Seif Shaban a.k.a Matonya. Anatarajiwa kufanya show jijini London sanjari na Nonini msanii anayefanya Genge kutokea nchini Kenya.



Show hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika TEREZA JOANNE BOAT KING GEORGE V DOCK E16 2QY London, United Kingdom. Inatarajiwa kuwa ya aina yake kutokana na umahiri wa wasanii hao wawili. Show imeandaliwa na BONGOUK PRESENT EAST AFRICAN SHOW DOWN 2010. Big up Matonya!!

TIMU YA SOKA YA WANAWAKE PONGWE KAMBINI!

TIMU ya soka ya wanawake Pongwe jana imeanza mazoezi yake katika uwanja wa soka Villa kwa ajili ya kujiandaa na michezo mbalimbali ya kirafiki. Akizungumza na Blog hii, Mkurugenzi wa timu hiyo Salim Baawazir amesema kuwa maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya michezo hiyo ya kirafiki yanaendelea vizuri.

Baawazir amesema kuwa timu hiyo itakutana na timu ya Tanga Women Fc katika mchezo ambao unatarajiwa kufanyika Pongwe ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa TRFA Said Sudi.

Ameongeza kuwa timu hiyo inatarajiwa kuelekea wilayani Pangani kwa ajili ya kushiriki michezo mbalimbali ya kirafiki.

Na Oscar Assenga, Pongwe.

"MBIO ZA BAISKELI TANGA OCTOKA 14"- SOPHIA WAKATI

(Sophia Wakati, mwandaaji wa mbio za baiskeli Tanga)

MKAKATI wa mashindano ya baiskeli inaendelea kupamba moto jijini hapa baada ya washiriki mbalimbali kujitokeza kuthibitisha kushiriki mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi october 14 mwaka huu mkoani hapa.

Akizungumza na Blog hii, mratibu wa michuano hiyo, Sophia Wakati amesema kuwa mpaka sasa tayari ameshaunda kamati ya watu watano wa kujadili mashindano hayo.

(Sophia Wakati akiwa na Oscar Assenga ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la Bingwa)

wakati amesema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na yamekwisha kamili ambapo kwa sasa wapo katika mkakati wa kutengeneza namba za washiriki ambapo zitakapo kamilika washiriki watakatiwa kupitia vituo mbalimbali vitavyowekwa jijini hapa.

Aidha amesema kuwa namba hizo zitawasaidia washiriki kutambulika katika mashindano hayo ambayo kwa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na msisimuko wa hali ya juu. Watakimbia kilomita 125 Kwa upande wa zawadi mshindi wa kwanza atapata 200,000,wa pili 150,000, wa tatu 100,000,wa nne 75,000 wa tano 50,000.

Mashindano hayo yatawashirikisha walemavu wa viungo ambayo watakimbia kilimeta 5 ambapo mshindi wa kwanza 100,000,mshindi wa pili 75,000,wa tatu 50,000.

Monday, September 27, 2010

VODACOM, SOFIA PRODUCTION RAHA TUPU TANGA!



Kampuni ya simu za mkononi Tanzania Vodacom, imefanya jambo la kihistoria mkoani Tanga baada ya kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa jijini hapa katika kuadhimisha miaka kumi ya kampuni hiyo kwenye uwanja wa Tangamano.


Shamrasharma hizo zilizoandaliwa na kampuni ya Sofia Production chini ya Aisha Kissoky na kudhaminiwa na Vodacom, pia ziliambatana na burudani kutoka kwa kundi zima la Zanzibar Stars ambao walikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa Taarab wanaotumia mtandao wa Vodacom. Burudani nyengine ni kutoka kwa Super Baikoko Bazoka, pamoja na vijana wa dansi wa Town Boys.

Umati ukishuhudia kinachoendelea wakati wa miaka kumi ya Vodacom Tanzania kunako uwanja wa Tangamano.

Msema chochote wa kundi la Zanzibar Stars alipkaribishwa kutangaza ratiba ya burudani.

Jumaa Kombo kutoka Sofia Production, akiwa kazini.

Vijana wa Vodacom wakiwa tayari kugawa zawadi kwa watumiaji wa mtandao huo waliokuwa wanajibu maswali ya papo kwa papo yaliyokuwa yanaulizwa uwanjani hapo.

Waimbaji nguli wa muziki wa Taarab nchini kutokea Zanzibar Stars...Jokha Kassim akiwa na mwenzake.

Kundi la Zanzibar Stars likiwa tayari kutoa burudani kwa wapenzi wake waliokuja kufurahi pamoja na kampuni ya Vodacom.

Waimbaji wa Zanzibar Stars wakishuka kwenye gari.

Hii ndio gari iliyowaleta kundi la Zanzibar Stars.

Anaitwa Mwagomero, ndio mwimbaji wa kundi la Super Baikoko Bazoka ya jijini Tanga. Mambo yao sio ya kawaida...ndio wanaongoza kwa Baikoko mkoani hapa!

Mimi (Anko Mo) nikiwa na mama Sofia Production, Aisha Kissoky ndie muandaaji wa shamrashamra hizo zilizodhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.

Huyu jamaa ndio alikuwa analeta raha zote....ni msema chochote wa shughuli nzima. Anaitwa Selemani Mtei.

Mwanadada kutoka kundi la Super Baikoko Bazoka, akifanya mambo yake. Anaiywa Halima.

Haya jamani..Tanga hiyoooo!! Nae kutoka Super Baikoko Bazoka, anaitwa Shakira akifanya mambo yake jukwaani.

Upande wa pili..umati ukishuhudiia mambo ya Vodacom Tanzania

Huduma zote za Vodacom Tanzania zilikuwepo kupitia vibanda hivi. Watu walipata kununua simcard pamoja na vocha zilizokuwa zinauzwa hapo. Hongera sana Vodacom Tanzania, pamoja na kampuni ya Sofia Production kwa kuleta mambo mazuri jijini Tanga.

Friday, September 24, 2010

"UMEACHANA NAE"- SADDY Q

Ngoma inaitwa 'Umeachana Nae'...anaitwa Saddy Q. Moja ya wasanii wanaofanya RnB ya kweli kutokea jijini Tanga. Sikiliza wimbo wake huo hapo juu kulia palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Week End njema wadu wa Vijimambo Vya Tanga!!

WATU WATANO WAKAMATWA NA GONGO KILINDI, TANGA!


Jeshi la polisi la mkoa Tanga linawashikilia watu wa tano kwa kosa la kukutwa lita 110 za pombe haramu ya gongo. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Liberatusi Sabasi amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 20 mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika Kijiji cha kwekivu wilayani Kilindi.

Sabasi amewataja watuhumiwa hao ni Adamu Aroni miaka 39, Bonge Mwanduro 52, Limbau Ndereko 58 wamekamatwa na lita 110 za gongo , Sila Mondo miaka 24, na Mbalazi Mtuka miaka 52 walikamatwa wakazi wa kijiji cha Kwekivu kitongoji cha Chanungwi wilayani Kilindi.

Kamanda huyo ameendelea kusema watuhumiwa wote ni wafanya biashara na wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

NIMR TANGA YATIMIZA MIAKA 30!

Mkuu wa mkoa wa Tanga Said Said Kalembo amesema kuwa magonjwa mengi yanayoikabili Tanzania yanahitaji mchango wa Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binaadamu NIMR katika kutafuta ufumbuzi wake pia amewasihi kupanua shughuli zao za utafiti kwa kuhusisha maeneo mengi yenye kipaumbele ukiacha malaria na utafiti wa virusi vya ukimwi pekee.

Ameyasema hayo wakati wa maonesho ya hadhara ya utafiti yanayojulikana kama OPEN DAY ya taasisi hiyo ya NIMR katika kituo chake kilichopo Mkabara na hospitali ya mkoa ya bombo mkoani Tanga hapo jana ikiwa ni maandalizi ya kutimiza miaka 30 yatakayofanyika 0ktoba mwaka tangu kuanzishwa kwake.

Aidha ameongeza kuwa NIMR mkoani hapa imebeba jukumu kubwa katika vituo malumu viavyotumika kufuatilia uwezo wa dawa za kutibu malaria na imefanya kazi na taasisi nyingine kwa karibu kutoa takwimu kwa wizara ya sfya na usitawi wa jamii kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti malaria (NMCP).

Ameongeza kuwa takwimu zilizopatiakana zilikuwa muhimu katika kufanya mabadiliko ya sera ya tiba ya malaria Tanzania ,na kuamini kuwa takwimu nyingi zitatolewa kwa kufuatilia dawa ya awali inayotumika kutibu malaria kwa sasa yaani ALU na nyinginezo.

Maabara hii pia inatoa msaada kwa program nyingine kama NLFP ambayo kiwango kilichopo kwa kutokomeza ugonjwa wa matende na mabusha hupimwa kwenye mbu kwa kutumia utalamu wa PCR ,aidha wataalamu wa maabara wa AMBRELA wanashiriki kupima malaria kimataifa kwa ajili ya kuangalia kiwango chao cha ubora katika kupima malaria kwenye utafiti ya chanjo ya RTS,S unaoendelea wilayani Korogwe.



'NITARUDISHA HESHIMA YA MKOA WA TANGA'- ASEMA LIPUMBA!

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amefufua matumiani ya wananchi wa Tanga na kuweka bayana kuwa atakapochaguliwa atahakikisha sekta ya viwanda mkoani Tanga inaimarika.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa Tanga katika uwanja wa Tangamano,Profesa Lipumba ameahidi kurejesha heshima ya Mkoa wa Tanga iliyoporomoka kwa viwanda vingi kufa huku ikishuka kwenye chati za mikoa maarufu kiuchumi kutoka nafasi ya pili hadi 16.

Amewaeleza wakazi wa Tanga kuwa atakapoingia madarakani atahakikisha hadhi ya Tanga inarudi kwa kuvifufua viwanda vilivyokufa na kueleza kuwa hayo yatawezekana ikiwa atachaguliwa kuingia ikulu.

Pia amezungumzia juu ya uboreshaji wa elimu hasa masomo ya sayansi kwa kuwawezesha kupatikana walimu watakaokuwa na uwezo wa kufundisha masomo hayo ili kuongeza idadi ya wanasayansi kwani ulimwengu huu ni wa sayansi.

Amewataka wananchi wa Tanga kuchagua madiwani wa chama hicho ili kuunda baraza la madiwani litakalosimamia fedha za miradi ya maendeleo ili wananchi waweze kunufaika na fedha hizo.

Awali Mgombea Ubunge wa CUF,Bw.Mussa Mbaruku amewataka wananchi kumpa kura ili kupata mtetezi wa kweli katika bunge kwani jimbo la Tanga kwa muda mrefu sasa limekosa uwakilishi wa kweli bungeni.


Thursday, September 23, 2010

MATUKIO KATIKA PICHA!

Mgombea ubunge wa jimbo la Korogwe mjini kupitia CCM,Yussph Nassir akizungumza na wanawake wa Wilaya ya Korogwe mara baada ya kupewa nafasi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kujinadi,mke huyo wa Rais alikuwa mjini hapa ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini ya kampeni.

Mke wa Mama Salma Kikwete akicheza wimbo wa pipii wa Marlow wakati akiwa katika mkutano wa ndani wa kampeni ya umnadi mumewe na wagombea wa ubunge na udiwani wa CCM uliofanyika ukumbi wa Mamba Club mjini Korogwe juzi.

Mbunge anayewakilisha walemavu Al Shaymaa Kwegyir akisakata rumba wakati wa mkutano uliohutubiwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete

Na Sussan Uhinga, Korogwe.

Wednesday, September 22, 2010

"NIPE STIKI"- ROMA, MC RISASI & BWI BWAX

Wimbo mpya kutoka kwa wasanii nguli wa muziki wa Hip Hop kutokea jijini Tanga Roma, Mc Risasi na Bwi Bwax....bonge moja la kolabo!!! Ngoma inaitwa "Nipe Stiki" Imetengenezwa pale King Falcom Production chini ya Producer Sam Chad. Fanya kama unausikiliza hivi hapo juu kulia palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!

MASTAA WA TANGA KIBAO NDANI YA FACEBOOK!!!